Leviticus 26:45 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
La! Kwa ajili yao nitalikumbuka agano nililofanya na wazee wao ambao niliwatoa katika nchi ya Misri, mataifa yakishuhudia, ili mimi niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
La! Kwa ajili yao nitalikumbuka agano nililofanya na wazee wao ambao niliwatoa katika nchi ya Misri, mataifa yakishuhudia, ili mimi niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka Agano langu na baba zao ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
La! Kwa ajili yao nitalikumbuka agano nililofanya na wazee wao ambao niliwatoa katika nchi ya Misri, mataifa yakishuhudia, ili mimi niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila kwa kuwatakia wokovu nitalikumbuka Agano, nililolifanya na baba zao wa kwanza nilipowatoa katika nchi ya Misri machoni pa wamizimu, niwe Mungu wao mimi Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapana! Kwa ajili yao nitakumbuka agano nililofanya na wazee wao ambao niliwatoa katika inchi ya Misri, mataifa yakishuhudia, kusudi mimi nikuwe Mungu wao. Mimi ni Yawe.