Leviticus 26:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kupura nafaka kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na uvunaji zabibu mpaka wakati wa kupanda mbegu. Mtakuwa na chakula tele na kuishi kwa usalama nchini mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupura nafaka kwenu kutaendelea hadi wakati wa kuvuna zabibu. Na kuvuna zabibu kutaendelea hadi wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kupura nafaka kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na uvunaji zabibu mpaka wakati wa kupanda mbegu. Mtakuwa na chakula tele na kuishi kwa usalama nchini mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuishi katika nchi yenu salama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kupura nafaka kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na uvunaji zabibu mpaka wakati wa kupanda mbegu. Mtakuwa na chakula tele na kuishi kwa usalama nchini mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, siku za kupura zitakapopokelewa na siku za kuchuma zabibu, nazo siku za hayo machumo zitapokelewa na siku za kupanda, nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, mkae katika nchi yenu na kutulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kupepeta ngano kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na mavuno ya zabibu mpaka wakati wa kupanda mbegu. Mutakuwa na chakula tele na kuishi kwa usalama katika inchi yenu.