Leviticus 27:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu akiiweka wakfu nyumba yake kuwa takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, kuhani ataamua thamani yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua, ndivyo itakavyokuwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu akiiweka wakfu nyumba yake kuwa takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, kuhani ataamua thamani yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua, ndivyo itakavyokuwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa BWANA, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo kama ni nzuri au mbaya. Thamani yo yote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa bwana, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA, ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu akiiweka wakfu nyumba yake kuwa takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, kuhani ataamua thamani yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua, ndivyo itakavyokuwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akiitakasa nyumba yake kuwa kipaji kitakatifu cha Bwana, mtambikaji na ayapime makombozi yake kwa kuipambanua kuwa njema au mbaya; nayo makombozi, mtambikaji atakayoyapima, yatakuwa yaleyale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akitakasa nyumba yake kuwa takatifu kwa Yawe, kuhani ataamua bei yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua, ndivyo itakavyokuwa.