Leviticus 27:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu akiiweka ardhi yake, ambayo ni urithi wake, wakfu kwa Mwenyezi-Mungu basi, thamani yake itapimwa kulingana na mbegu zinazotumika kulipanda shamba hilo; kwa kila kilo ishirini za shayiri thamani yake itakuwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mtu ataweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa Mwenyezi Mungu, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kama mtu akiweka wakfu kwa Bwana sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu akiiweka ardhi yake, ambayo ni urithi wake, wakfu kwa Mwenyezi-Mungu basi, thamani yake itapimwa kulingana na mbegu zinazotumika kulipanda shamba hilo; kwa kila kilo ishirini za shayiri thamani yake itakuwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa BWANA, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa bwana, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kama mtu akiweka wakfu kwa BWANA sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu akiiweka ardhi yake, ambayo ni urithi wake, wakfu kwa Mwenyezi-Mungu basi, thamani yake itapimwa kulingana na mbegu zinazotumika kulipanda shamba hilo; kwa kila kilo ishirini za shayiri thamani yake itakuwa shekeli hamsini za fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akitakasa kipande cha shamba lililo fungu lake kuwa mali ya Bwana, utayapima makombozi yake kwa kipimo cha mbegu zinazoenea hapo: kama hicho kipande cha shamba kinataka mbegu za mawele frasila kumi makombozi yake ni fedha hamsini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kama mtu akiweka wakfu kwa BWANA sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akitakasa shamba lake, ambalo ni urizi wake, kwa ajili ya Yawe, basi, bei yake itapimwa kulingana na mbegu zinazotumiwa kwa kupanda shamba hilo. Kwa kila kilo makumi mbili za shayiri bei yake itakuwa shekeli makumi tano za feza.