Leviticus 27:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini kitu chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, kiwe ni mtu au mnyama au kitu kilichopatikana kwa urithi, hakitauzwa wala kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu ni kitakatifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu cho chote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa Bwana, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini kitu chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, kiwe ni mtu au mnyama au kitu kilichopatikana kwa urithi, hakitauzwa wala kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu ni kitakatifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini cho chote kile mtu alichonacho na kukitoa kwa BWANA, ikiwa ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, chaweza kuuzwa au kukombolewa; cho chote kilichotolewa ni kitakatifu sana kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu kwa bwana, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu chochote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini kitu chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, kiwe ni mtu au mnyama au kitu kilichopatikana kwa urithi, hakitauzwa wala kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu ni kitakatifu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yo yote, mtu atakayomtolea Bwana kuwa yake kwa kuyatia mwiko wa kutunzwa na mtu, akiyatoa katika yo yote yaliyo yake yeye, kama ni mtu au nyama wa kufuga au shamba lililo la fungu lake mwenyewe, hayawezekani wala kuuzwa wala kukombolewa, maana yote pia yaliyotiwa mwiko wa kutunzwa na mtu ni matakatifu yenyewe, ni yake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu cho chote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kitu chochote kilichotakaswa kwa Yawe, kama ni mutu au nyama au kitu kilichopatikana kwa urizi, hakitauzishwa wala kukombolewa. Chochote kilichotakaswa kwa Yawe ni kitakatifu kabisa.