Leviticus 27:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanamume wa miaka ishirini hadi miaka sitini atakombolewa kwa fedha shekeli 50 kulingana na kipimo cha mahali patakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hesabu yako itakuwa kwa mtu mume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanamume wa miaka ishirini hadi miaka sitini atakombolewa kwa fedha shekeli 50 kulingana na kipimo cha mahali patakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
thamani ya mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini atakombolewa kwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hesabu yako itakuwa kwa mwanamume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanamume wa miaka ishirini hadi miaka sitini atakombolewa kwa fedha shekeli 50 kulingana na kipimo cha mahali patakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho kipimo chako ni hiki: mtu mume aliye wa miaka ishirini mpaka sitini makombozi yake, utakayompimia, ni fedha hamsini, zikipimwa na mizani ya Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hesabu yako itakuwa kwa mtu mume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanaume wa miaka makumi mbili mpaka miaka makumi sita atakombolewa kwa feza shekeli makumi tano kulingana na kipimo cha Pahali Patakatifu.