Leviticus 27:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote hana ruhusa kuuliza kama mnyama huyo ni mzuri au mbaya wala mnyama huyo kamwe hatabadilishwa kwa mwingine. Kama akibadilishwa kwa mwingine, wanyama wote wawili watakuwa watakatifu; hawatakombolewa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Akimbadili, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hataangalia kwamba ni mwema au kwamba ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yo yote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote hana ruhusa kuuliza kama mnyama huyo ni mzuri au mbaya wala mnyama huyo kamwe hatabadilishwa kwa mwingine. Kama akibadilishwa kwa mwingine, wanyama wote wawili watakuwa watakatifu; hawatakombolewa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hataangalia kama ni mwema au ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yoyote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote hana ruhusa kuuliza kama mnyama huyo ni mzuri au mbaya wala mnyama huyo kamwe hatabadilishwa kwa mwingine. Kama akibadilishwa kwa mwingine, wanyama wote wawili watakuwa watakatifu; hawatakombolewa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo watu wasitazame sana, kama ni mwema au kama ni mbaya, wala wasimbadilishe. Kam mtu anambadilisha, yule wa kwanza pamoja na badili yake watakuwa wote wawili mali takatifu za Bwana, wasiwezekane kukombolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hataangalia kwamba ni mwema au kwamba ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yo yote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote hana ruhusa ya kuuliza kama nyama huyo ni muzuri au mubaya wala nyama huyo hatabadilishwa na mwingine. Kama akibadilishwa na mwingine, nyama wote wawili watakuwa watakatifu. Hawatakombolewa.