Leviticus 27:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini na hawezi kulipa gharama yake, basi, mtu huyo atapelekwa kwa kuhani. Kuhani atampima thamani yake kulingana na uwezo wa huyo aliyeweka nadhiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile yule anayeweka nadhiri anaweza kulipa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamtia kima; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomtia kima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini na hawezi kulipa gharama yake, basi, mtu huyo atapelekwa kwa kuhani. Kuhani atampima thamani yake kulingana na uwezo wa huyo aliyeweka nadhiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu ye yote anayeweka nadhiri ni maskini mno kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akiwa ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamkadiria; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomkadiria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini na hawezi kulipa gharama yake, basi, mtu huyo atapelekwa kwa kuhani. Kuhani atampima thamani yake kulingana na uwezo wa huyo aliyeweka nadhiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama ni mkosefu wa mali, asiweze kuyalipa hayo makombozi, uliyompimia, na wamsimamishe mbele ya mtambikaji, naye mtambikaji na ampimie makombozi yake akiyalinganisha na mali, yule mwenye kuapa anazoweza kuzipata kwa mkono wake; hicho kiwe kipimo chake mtambikaji cha kumpimia hayo makombozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamtia kima; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomtia kima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiwa mutu huyu ni masikini na hawezi kulipa malipo yake, basi, mutu yule atapelekwa kwa kuhani. Kuhani atapima bei yake kulingana na uwezo wa huyo aliyefanya kiapo.