Leviticus 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mtu anatoa sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng'ombe kutoka katika kundi, akiwa dume au jike, atamleta huyo mbele za BWANA mnyama asiye na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama toleo lake ni ng'ombe ya tambiko ya shukrani, aliyoitoa katika ng'ombe wake, kama ni wa kiume au wa kike, sharti apeleke asiye na kilema, apate kumtoa mbele ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu anatoa sadaka ya amani na sadaka yake ni ngombe dume au dike, nyama huyo asikuwe na kilema mbele yangu.