Leviticus 3:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mbele ya hema la mkutano. Wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mbele ya hema la mkutano. Wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mbele ya hema la mkutano. Wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha aubandike mkono wake kichwani pake, amchinje mbele ya Hema la Mkutano, nayo damu yake wana wa Haroni na wainyunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akiweka mukono wake juu ya kichwa cha nyama huyo na kumuchinja mbele ya hema la mukutano. Wazao wa Haruni watanyunyizia mazabahu damu yake pande zake zote.