Leviticus 3:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa Aroni wataiteketeza madhabahuni pamoja na sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni; hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wana wa Haruni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyo juu ya kuni zinazowaka; ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Aroni wataiteketeza madhabahuni pamoja na sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni; hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wana wa Haruni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa Aroni wataiteketeza madhabahuni pamoja na sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni; hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wana wa Haroni na wayachome moto mezani pa kutambikia juu ya ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima iliyowekwa juu ya kuni zilizopangwa motoni; huu ndio moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Haruni wataiteketeza juu ya mazabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa inayokuwa juu ya kuni. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.