Leviticus 3:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama sadaka hiyo ya kufanya amani unayomtolea Mwenyezi-Mungu ni kutoka kundi la kondoo au mbuzi, basi achaguliwe dume au jike asiye na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kuwa sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia Bwana, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama sadaka hiyo ya kufanya amani unayomtolea Mwenyezi-Mungu ni kutoka kundi la kondoo au mbuzi, basi achaguliwe dume au jike asiye na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka katika kundi kama sadaka ya amani kwa BWANA, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama sadaka hiyo ya kufanya amani unayomtolea Mwenyezi-Mungu ni kutoka kundi la kondoo au mbuzi, basi achaguliwe dume au jike asiye na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama ng'ombe yake ya tambiko, anayotaka kumtolea Bwana, ameitoa katika mbuzi au kondoo, kama ni wa kiume au wa kike, sharti apeleke asiye na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama sadaka hiyo ya amani unayomutolea Yawe ni kutoka kundi la kondoo au mbuzi, basi achaguliwe dume au dike asiyekuwa na kilema.