Leviticus 3:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, kutoka katika sadaka hiyo ya amani anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atamtolea sehemu zifuatazo: Mafuta yake, mkia wenye mafuta mzima uliokatwa karibu kabisa na uti wa mgongo pamoja na mafuta yote yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo kwenye matumbo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa Bwana, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, kutoka katika sadaka hiyo ya amani anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atamtolea sehemu zifuatazo: mafuta yake, mkia wenye mafuta mzima uliokatwa karibu kabisa na uti wa mgongo pamoja na mafuta yote yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo kwenye matumbo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa BWANA kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa BWANA, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, kutoka katika sadaka hiyo ya amani anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atamtolea sehemu zifuatazo: Mafuta yake, mkia wenye mafuta mzima uliokatwa karibu kabisa na uti wa mgongo pamoja na mafuta yote yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo kwenye matumbo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha na atoe katika kondoo aliyechinjwa kuwa ng'ombe ya tambiko ya shukrani vile vipande vya kumchomea Bwana kwa moto, ni mafuta yake: mkia wenye mafuta, wote mzima auondoe kwa kuukata hapo, ulipoungwa na mifupa ya mgongoni, tena yale mafuta yanayoufunika utumbo pamoja na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa BWANA, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, kutoka katika sadaka hiyo ya amani Yawe anayotolewa kwa moto, atamutolea sehemu hizi: mafuta yake, mukia muzima wenye mafuta uliokatwa karibu kabisa na uti wa mugongo pamoja na mafuta yote yanayofunika matumbotumbo na mafuta yote yanayokuwa kwenye matumbotumbo,