Leviticus 4:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi hadi mahali palipo safi, ambapo majivu hutupwa; naye atamchoma kwa moto wa kuni juu ya lundo la majivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maana, huyo ng'ombe mzima atamchukua nje ya marago hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi mpaka mahali palipo safi kiibada, ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni zilizoko juu ya lundo la majivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi mpaka mahali palipo safi kiibada, ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni zilizoko juu ya lundo la majivu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maana, huyo ng'ombe mzima atamchukua nje ya kambi hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
haya yote pia ya huyu dume sharti ayatoe nje ya makambi na kuyapeleka mahali panapotakata, wanapomwagia majivu ya mafuta; ndipo ayaweke juu ya kuni, ayateketeze moto. Sharti yateketezwe papo hapo, wanapomwagia majivu ya mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maana, huyo ng’ombe mzima atamchukua nje ya marago hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ni kusema ngombe muzima aliyebakia atamupeleka na kumuteketeza inje ya kambi pahali safi ambapo majivu yanatupwa, naye atamuchoma kwa moto juu ya kuni. Atachomwa kwa moto pale pahali pa kumwangia majivu.