Leviticus 4:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu, hata kama jumuiya hawafahamu jambo hilo, wana hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na Bwana, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yo yote ya BWANA, hata kama jumuiya haifahamu juu ya jambo hilo, wana hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya bwana, hata kama jumuiya haifahamu juu ya jambo hilo, wana hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likafichika machoni pa huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkutano wote wa Waisiraeli wakikosa neno, isipokuwa kwa kusudi, nalo hilo neno halikujulikana machoni pao wote, ya kuwa wamelikosea agizo moja tu katika maagizo yote ya Bwana wakifanya yasiyofanywa, basi, kama wamekora manza hivyo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa Waisraeli wote pamoja wametenda zambi bila kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Yawe,