Leviticus 4:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanapotambua dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko walete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi, na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hapo itakapojulikana hiyo dhambi waliyoifanya, ndipo mkutano utatoa ng'ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi, na kumleta mbele ya hema ya kukutania.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanapotambua juu ya dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko lilete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanapotambua kuhusu dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko lilete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hapo itakapojulikana hiyo dhambi waliyoifanya, ndipo mkutano utatoa ng'ombe dume mchanga awe sadaka ya dhambi, na kumleta mbele ya hema ya kukutania.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hapo kosa lao, walilolikosa, litakapojulikana, wao wa mkutano na watoe dume la ng'ombe aliye mwana bado kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wamfikishe mbele ya Hema la Mkutano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hapo itakapojulikana hiyo dhambi waliyoifanya, ndipo mkutano utatoa ng’ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi, na kumleta mbele ya hema ya kukutania.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mara tu zambi hiyo itakapojulikana, watatoa ngombe dume muchanga akuwe sadaka kwa ajili ya zambi. Watamuleta kwenye hema la mukutano.