Leviticus 4:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha beberu na kumchinjia mahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale sadaka za kuteketezwa huchinjiwa mbele za Mwenyezi Mungu. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana; ni sadaka ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha beberu na kumchinjia mahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale ambapo sadaka za kuteketezwa huchinjwa mbele za BWANA. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale ambapo sadaka za kuteketezwa huchinjiwa mbele za bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha beberu na kumchinjia mahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha na aubandike mkono wake kichwani pake huyo dume, kisha amchinje mahali hapo, wanapochinja mbele ya Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima; hivyo naye atakuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ataweka mukono wake juu ya kichwa cha beberu na kumuchinjia pahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Yawe. Hiyo ni sadaka kwa ajili ya zambi.