Leviticus 4:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza, na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha kuhani atatwaa katika damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza, na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha kuhani atatwaa baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtambikaji na atwae damu nyingine ya huyu ng'ombe ya tambiko ya weuo kwa kidole chake, azipake pembe za meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, nayo damu yake nyingine aimwagie misingi ya meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha kuhani atatwaa katika damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka kwa ajili ya zambi na kuipakaa kwenye pembe za mazabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwanga chini kwenye tako la mazabahu ya kuteketezea sadaka.