Leviticus 4:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza madhabahuni, kama afanyavyo na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamfanyia mtawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu, kama alivyoteketeza mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza madhabahuni, kama afanyavyo na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamfanyia mtawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu kama alivyoteketeza mafuta ya sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu, kama alivyoteketeza mafuta ya sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza madhabahuni, kama afanyavyo na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamfanyia mtawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mafuta yake yote na ayachome moto mezani pa kutambikia kama mafuta ya ng'ombe ya tambiko ya shukrani. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kosa lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza juu ya mazabahu, kama vile anavyofanya na mafuta ya nyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamufanyia mutawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya zambi yake, naye atasamehewa.