Leviticus 4:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama aondoavyo mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, naye kuhani atayateketeza madhabahuni, na harufu yake nzuri itampendeza Mwenyezi-Mungu. Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama aondoavyo mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, naye kuhani atayateketeza madhabahuni, na harufu yake nzuri itampendeza Mwenyezi-Mungu. Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza BWANA. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza bwana. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama aondoavyo mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, naye kuhani atayateketeza madhabahuni, na harufu yake nzuri itampendeza Mwenyezi-Mungu. Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mafuta yake yote na ayaondoe, kama mafuta yanavyoondolewa katika ng'ombe ya tambiko ya shukrani. Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia, yawe mnuko wa kumpendeza Bwana. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kosa lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama vile anavyoondoa mafuta ya nyama wa sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya mazabahu, na harufu yake nzuri itamupendeza Yawe. Basi, kuhani atamufanyia yule mutu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.