Leviticus 5:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamletea kuhani, naye atachukua unga huo konzi moja na kuuteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamletea kuhani, naye atachukua unga huo konzi moja na kuuteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atauleta kwa kuhani, naye atauchukua unga huo konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamletea kuhani, naye atachukua unga huo konzi moja na kuuteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiupeleka kwa mtambikaji, huyo mtambikaji na achukue humo wa kulijaza gao lake, uwe wa kumkumbushia Bwana, akiuchoma moto hapo pa kutambikia juu ya mioto ya Bwana. Hivyo nao utakuwa kipaji cha tambiko cha weuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atamuletea kuhani, naye atatwaa unga huo mukono mumoja na kuuteketeza juu ya mazabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Hiyo ni sadaka kwa ajili ya zambi.