Leviticus 5:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama mtu yeyote akikosa kwa kutenda dhambi bila kujua kuhusu kutotoa vitu vitakatifu anavyotolewa Mwenyezi-Mungu, atamletea kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake. Wewe utapima thamani yake kulingana na kipimo rasmi cha mahali patakatifu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Mwenyezi Mungu, huyo mtu ataleta kwa Mwenyezi Mungu kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari, na mwenye thamani halisi ya fedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya Bwana; ndipo atakapomletea Bwana sadaka yake ya hatia, kondoo mume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama mtu yeyote akikosa kwa kutenda dhambi bila kujua kuhusu kutotoa vitu vitakatifu anavyotolewa Mwenyezi-Mungu, atamletea kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake. Wewe utapima thamani yake kulingana na kipimo rasmi cha mahali patakatifu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya BWANA, huyo mtu ataleta kwa BWANA kama adhabu, kondoo dume mmoja kutoka katika kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya bwana, huyo mtu ataleta kwa bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo dume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama mtu yeyote akikosa kwa kutenda dhambi bila kujua kuhusu kutotoa vitu vitakatifu anavyotolewa Mwenyezi-Mungu, atamletea kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake. Wewe utapima thamani yake kulingana na kipimo rasmi cha mahali patakatifu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akilivunja Agano, akikosa kwa kuchukua kitu kilicho mali ya Bwana, asipovijua, na ampelekee Bwana ng'ombe yake ya tambiko ya upozi, akitoa katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona kuwa wa fedha mbili tatu zilizopimwa kwa kipimo cha Patakatifu; huyo atakuwa ng'ombe yake ya tambiko ya upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo mume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu yeyote akikosa kwa kutenda zambi bila kujua juu ya kutokutoa vitu vitakatifu Yawe anavyotolewa, atamuletea kondoo dume asiyekuwa na kilema kutoka kundi lake. Wewe utapima bei yake kulingana na kipimo cha Pahali Patakatifu. Hiyo ni sadaka kwa ajili ya kosa.