Leviticus 5:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama mtu akifanya dhambi, na kutenda yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia vivyo, naye atachukua uovu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za BWANA, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za bwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata mtu akikosea agizo lo lote la Bwana, ijapo ni moja tu, kwa kufanya yasiyofanywa, asipovijua, naye atakuwa amekora manza, nao uovu wake utamkalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia vivyo, naye atachukua uovu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote akitenda zambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Yawe, yeye ana kosa, na atalipa azabu ya kosa lake.