Leviticus 5:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamletea kuhani kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake akiwa na thamani sawa na ile ya sadaka ya hatia. Na kuhani atamfanyia upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ataleta kondoo mume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamletea kuhani kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake akiwa na thamani sawa na ile ya sadaka ya hatia. Na kuhani atamfanyia upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ataleta kondoo dume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamletea kuhani kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake akiwa na thamani sawa na ile ya sadaka ya hatia. Na kuhani atamfanyia upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo na atoe katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona, ya kama anatosha kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi. Kisha ampeleke kwa mtambikaji, naye mtambikaji atampatia upozi kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa pasipo kulijua kuwa ni kosa; naye akiwa hakuvijua kweli ataondolewa kosa lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ataleta kondoo mume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atamuletea kuhani kondoo dume asiyekuwa na kilema kutoka kundi lake ikiwa na bei sawa na ile ya sadaka ya kosa. Na kuhani atamufanyia ibada ya upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa.