Leviticus 5:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Au mtu akitambua kuwa ana hatia, kama vile akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vinavyotambaa ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, kama ni mzoga wa mnyama wa nyikani aliye najisi, au kama ni mzoga wa mnyama wa mfugo aliye najisi, au kama ni mzoga wa mdudu aliye najisi, naye jambo hilo linamfichamania, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Au kama mtu akigusa kitu cho chote ambacho si safi kwa kawaida ya ibada, kama ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata kama hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Au kama mtu akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni mzoga wa mnyama nyikani aliye najisi, au ni mzoga wa mnyama afugwae aliye najisi, au ni mzoga wa mdudu aliye najisi, bila kujua, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au hivi: mtu akigusa cho chote kisichotakata, kama ni mzoga wa nyama chafu wa porini au mzoga wa nyama chafu wa kufugwa au mzoga wa dudu chafu, asijue, ya kuwa amejipatia uchafu, basi, naye ni mwenye manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, kama ni mzoga wa mnyama wa nyikani aliye najisi, au kama ni mzoga wa mnyama wa mfugo aliye najisi, au kama ni mzoga wa mdudu aliye najisi, naye jambo hilo linamfichamania, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Au kama mutu yeyote kati yenu akijichafua bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote kichafu, ikuwe ni muzoga wa nyama wa pori au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na kosa.