Leviticus 5:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Au akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu uwao wote ambao kwa huo amepata unajisi, na jambo hilo linamfichamania, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu cho chote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata ikiwa hana habari juu yake, atakapojua atakuwa ana hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu wowote ambao kwao amepata unajisi, bila kujua, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au hivi: mtu akigusa uchafu wo wote wa mtu au kichafu cho chote, basi, hapo atakapokijua atakuwa ni mwenye manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu uwao wote ambao kwa huo amepata unajisi, na jambo hilo linamfichamania, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Au mutu akigusa kitu chochote toka kwa mwanadamu kinachohesabiwa kuwa kichafu, kikuwe kile ambacho kinamufanya mutu kuwa muchafu bila kujua, basi, atakapojua atakuwa na kosa.