Leviticus 5:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, ni lazima alete kwa Mwenyezi Mungu kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kwa ajili ya adhabu ya dhambi aliyoitenda lazima alete kwa BWANA kondoo jike au mbuzi kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, lazima alete kwa bwana kondoo jike au mbuzi jike kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo jike, au mbuzi jike, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha ampelekee Bwana malipo ya manza zake, alizozikora kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa, akitoa katika kundi lake jike la kondoo au la mbuzi kwa ajili ya kosa lake. Ndipo, mtambikaji atakapompatia upozi, aondolewe kosa lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kumuletea Yawe sadaka yake kwa ajili ya kosa. Kwa ajili ya zambi aliyotenda ataleta kondoo dike au mbuzi dike kutoka kundi lake amutoe sadaka kwa ajili ya zambi. Naye kuhani atamufanyia ibada ya upatanisho kwa ajili ya zambi yake.