Leviticus 5:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: Mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini kama huyo mtu hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda wawili wa njiwa kwa Mwenyezi Mungu ikiwa ni adhabu kwa ajili ya dhambi yake: mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea Bwana hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa BWANA kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa bwana kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: Mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkono wake usipomfikilia kondoo, na ampelekee Bwana hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga kuwa ng'ombe yake ya tambiko ya weuo kwa ajili ya hilo kosa, alilolikosa, mmoja wa weuo, mmoja wa kuteketezwa nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama hawezi kutoa mwana-kondoo wa sadaka ya kosa kwa ajili ya zambi aliyotenda, basi atamuletea Yawe hua wawili au vitoto viwili vya njiwa, mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto.