Leviticus 5:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikining’inia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamkongonyoa kichwa shingoni mwake, lakini asimpasue vipande viwili;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake na kuacha kichwa chake kikining'inia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikining’inia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamnyonga shingo na kuvunja kichwa chake, lakini asimpasue vipande viwili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiwapeleka kwa mtambikaji, huyo atatoa kwanza yule wa weuo akivunja kichwa chake hapo, kinaposhikamana na shingo, lakini hatakiondoa kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamkongonyoa kichwa shingoni mwake, lakini asimpasue vipande viwili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamutoa mumoja akuwe sadaka kwa ajili ya zambi kwa kumukongonyoa shingo yake bila kuachanisha kichwa chake.