Leviticus 6:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha kuhani akiwa amevaa vazi lake rasmi la kitani na kaptura yake ya kitani, atachukua majivu ya ile sadaka kutoka madhabahuni na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani mwilini wake, na aondoe majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu, na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha kuhani akiwa amevaa vazi lake rasmi la kitani na kaptura yake ya kitani, atachukua majivu ya ile sadaka kutoka madhabahuni na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za kitani za ndani, kisha ataondoa majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani mwilini wake, na aondoe majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu, na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha kuhani akiwa amevaa vazi lake rasmi la kitani na kaptura yake ya kitani, atachukua majivu ya ile sadaka kutoka madhabahuni na kuyaweka kando ya madhabahu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji na avae vazi lake la ukonge, hata suruali za ukonge na avae mwilini wake, nayo majivu ya ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima yaliyopo hapo juu ya meza ya kutambikia ayazoe, ayaweke kando ya meza ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usipikwe hata kidogo pamoja na chachu. Nimewapa wao sehemu hiyo kutoka sadaka wanazonitolea kwa moto. Ni sadaka takatifu kabisa kama vile sadaka kwa ajili ya zambi na kwa ajili ya kosa zinavyokuwa.