Leviticus 6:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wa makuhani atachukua konzi moja ya unga wa sadaka ya nafaka pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho; harufu yake itampendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atachukua konzi moja ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulio juu ya sadaka ya nafaka, na kuteketeza sehemu hiyo ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atatwaa konzi yake katika huo unga, katika huo unga mwembamba wa sadaka ya unga, na katika mafuta yake, na ubani wote ulio juu ya sadaka ya unga, kisha atauteketeza juu ya madhabahu kuwa harufu ya kupendeza, kuwa ukumbusho wake kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wa makuhani atachukua konzi moja ya unga wa sadaka ya nafaka pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho; harufu yake itampendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote juu ya sadaka ya nafaka na kuteketeza sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulioko juu ya sadaka ya nafaka, ateketeze sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atatwaa konzi yake katika huo unga, katika huo unga mwembamba wa sadaka ya unga, na katika mafuta yake, na ubani wote ulio juu ya sadaka ya unga, kisha atauteketeza juu ya madhabahu kuwa harufu ya kupendeza, kuwa ukumbusho wake kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wa makuhani atachukua konzi moja ya unga wa sadaka ya nafaka pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho; harufu yake itampendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha atanyanyua katika unga mwembamba wa kilaji cha tambiko wa kulijaza gao lake pamoja na mafuta yake na uvumba wote ulioko juu ya kilaji cha tambiko, auvukize mezani pa kutambikia, uwe mnuko upendezao wa kumkumbushia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atatwaa konzi yake katika huo unga, katika huo unga mwembamba wa sadaka ya unga, na katika mafuta yake, na ubani wote ulio juu ya sadaka ya unga, kisha atauteketeza juu ya madhabahu kuwa harufu ya kupendeza, kuwa ukumbusho wake kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani anayekuwa muzao wa Haruni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamutolea Yawe sadaka hiyo. Hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa kwa moto.