Leviticus 6:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unga uliosalia atakula Aroni na wazawa wake makuhani bila kutiwa chachu. Wataula kwenye mahali patakatifu uani mwa hema la mkutano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, nao wataila katika ua wa Hema la Kukutania.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na unga uliosalia Haruni na wanawe wataula; utaliwa pasipo kutiwa chachu, katika mahali patakatifu; katika ua wa hema ya kukutania ndipo watakapoula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unga uliosalia atakula Aroni na wazawa wake makuhani bila kutiwa chachu. Wataula kwenye mahali patakatifu uani mwa hema la mkutano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aroni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, wataila kwenye ua wa Hema la Kukutania.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, nao wataila kwenye ua wa Hema la Kukutania.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na unga uliosalia Haruni na wanawe wataula; utaliwa pasipo kutiwa chachu, katika mahali patakatifu; katika ua wa hema ya kukutania ndipo watakapoula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unga uliosalia atakula Aroni na wazawa wake makuhani bila kutiwa chachu. Wataula kwenye mahali patakatifu uani mwa hema la mkutano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao unga utakaosalia wataula Haroni na wanawe, uliwe hapo mahali patakatifu pasipo kutiwa chachu; waule uani penye Hema la Mkutano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na unga uliosalia Haruni na wanawe wataula; utaliwa pasipo kutiwa chachu, katika mahali patakatifu; katika ua wa hema ya kukutania ndipo watakapoula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sadaka yoyote ya ngano iliyotolewa na kuhani itateketezwa yote; haitakuliwa hata kidogo.