Leviticus 6:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mwanaume mzao wa Haruni aweza kuila. Ni fungu lake milele la sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mwana mume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya Bwana yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu awaye yote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mwanaume mzao wa Aroni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa moto kwa vizazi vijavyo. Cho chote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mwanaume mzao wa Haruni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwa bwana kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mwanamume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu yeyote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Haroni wote walio wa kiume wataula; hii na iwe haki ya kale na kale ya vizazi vyenu kuupata kwenye mioto ya Bwana. Kila atakayeugusa sharti awe ametolewa kuwa mtakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mwana mume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu awaye yote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umwambie Haruni na wana wake kwamba hii ndiyo sheria ya ibada kuelekea sadaka kwa ajili ya zambi, pahali ambapo nyama wa sadaka ya kuteketezwa anapochinjiwa ndipo atakapochinjiwa nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi, mbele ya Yawe. Hiyo ni sadaka takatifu kabisa.