Leviticus 6:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unga huo utachanganywa na mafuta na kuokwa; kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumtolea Mwenyezi-Mungu; na harufu ya sadaka yake itampendeza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utaandaliwa kaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unga huo utachanganywa na mafuta na kuokwa; kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumtolea Mwenyezi-Mungu; na harufu ya sadaka yake itampendeza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utaandaliwa kikaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowana utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unga huo utachanganywa na mafuta na kuokwa; kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumtolea Mwenyezi-Mungu; na harufu ya sadaka yake itampendeza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti uandaliwe kaangoni na kutiwa mafuta kuwa vitumbua. Kisha avipeleke na kuvimega vipandevipande; hivi ndivyo vilaji vya tambiko, utakavyovitoa, viwe mnuko wa kumpendeza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utaandaliwa kaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sadaka hiyo ikipikiwa katika vyombo vya udongo, vyombo hivyo vitavunjwa. Lakini ikiwa vyombo hivyo ni vya shaba, basi, vitasafishwa vizuri kwa maji.