Leviticus 6:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyepakwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la milele la Mwenyezi Mungu, nalo litateketezwa kabisa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa Bwana kwa amri ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtoto atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la BWANA, nalo litateketezwa kabisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la bwana, nalo litateketezwa kabisa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa BWANA kwa amri ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji aliyepakwa mafuta mahali pake Haroni miongoni mwa wanawe ndiye atakayevitoa; hii na iwe haki ya kale na kale ya Bwana, navyo sharti vichomwe moto vyote vizima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa BWANA kwa amri ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanaoruhusiwa kuikula ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao kwa vile hiyo ni sadaka takatifu kabisa.