Leviticus 6:25 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwambie Aroni na wanawe kuwa ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa dhambi, mahali pale ambapo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa ndipo atakapochinjiwa mnyama wa sadaka ya kuondoa dhambi, mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwambie Haruni na wanawe: ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za Mwenyezi Mungu mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa; ni takatifu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za Bwana; ni takatifu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwambie Aroni na wanawe kuwa ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa dhambi, mahali pale ambapo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa ndipo atakapochinjiwa mnyama wa sadaka ya kuondoa dhambi, mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwambie Aroni na wanawe: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjwa mbele za BWANA mahali sadaka ya kuteketezwa ichinjiwapo, ni takatifu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwambie Haruni na wanawe: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za bwana mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, ni takatifu sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za BWANA; ni takatifu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwambie Aroni na wanawe kuwa ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa dhambi, mahali pale ambapo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa ndipo atakapochinjiwa mnyama wa sadaka ya kuondoa dhambi, mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwambie Haroni na wanawe: Haya ndiyo maongozi ya ng'ombe za tambiko za weuo: mahali hapo, ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima zinapochinjwa, nazo ng'ombe za tambiko za weuo zichinjwe papo hapo mbele ya Bwana, maana nazo ni takatifu zenywe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za BWANA; ni takatifu sana.