Leviticus 6:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
au amepata kitu cha jirani yake kilichopotea, akasema kwamba hakukiona, au ameapa uongo juu ya chochote ambacho watu hufanya wakawa na hatia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
au akiokota mali iliyopotea na akadanganya kuihusu, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu wanaweza kuitenda;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
au amepata kitu cha jirani yake kilichopotea, akasema kwamba hakukiona, au ameapa uongo juu ya chochote ambacho watu hufanya wakawa na hatia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
au akiokota mali iliyopotea na akadanganya au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yo yote ambayo watu waweza kuitenda;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
au akiokota mali iliyopotea na akadanganya, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu waweza kuitenda;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
au kupata kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
au amepata kitu cha jirani yake kilichopotea, akasema kwamba hakukiona, au ameapa uongo juu ya chochote ambacho watu hufanya wakawa na hatia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
au akiokota kitu kilichopotea na kuvibisha na kuapa kiapo cha uwongo, akiwa amekosa moja tu katika mambo haya, watu wanayoyakosa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuhani akiwa amevaa nguo yake ya kitani na kapitula yake ya kitani, atatwaa majivu ya ile sadaka kutoka juu ya mazabahu na kuyaweka kando ya mazabahu.