Leviticus 6:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
au cho chote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, aongeze sehemu ya tano ya thamani yake na kumpa vyote mwenye mali siku ile anapopeleka sadaka yake ya hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
au kitu chochote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nayo yote, aliyoyachukua kwa kuapa kiapo cha uwongo, yote pia ayalipe swasawa, kama yalivyokuwa, kisha sharti aongeze fungu la tano. Sharti mpe yeye aliye mwenye mali hizo siku hiyo, atakapotoa ng'ombe yake ya tambiko ya upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Moto wa mazabahu lazima uendelee kuwaka wala usizimike. Kila siku asubui kuhani ataweka kuni kwenye moto huo na juu yake atapanga sadaka ya kuteketezwa, mbele ya kuteketeza mafuta ya sadaka ya amani.