Leviticus 6:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye atasamehewa kosa ambalo alikuwa amelifanya.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu, naye atasamehewa kwa kosa lolote katika mambo aliyoyatenda lililomfanya kuwa na hatia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye atasamehewa kosa ambalo alikuwa amelifanya.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa kwa kosa lo lote katika mambo hayo aliyoyatenda yaliyomfanya kuwa na hatia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za bwana, naye atasamehewa kwa kosa lolote katika mambo hayo aliyoyatenda yaliyomfanya kuwa na hatia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa; katika jambo lolote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye atasamehewa kosa ambalo alikuwa amelifanya.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji atampatia upozi mbele ya Bwana; ndipo, atakapoondolewa kosa lake, alilolikosa kuliko mengine yote kwa kukora zile manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndio sheria juu ya ibada inayoelekea sadaka ya vyakula. Wazao wa Haruni ndio wanaokuwa na uwezo wa kumutolea Yawe sadaka hiyo juu ya mazabahu.