Leviticus 7:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumshukuru Mungu italiwa siku hiyohiyo inapotolewa; hataacha hata sehemu yake hadi asubuhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku hiyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote hadi asubuhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwa ajili ya shukrani italiwa siku iyo hiyo ya matoleo yake; asisaze yo yote hata asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumshukuru Mungu italiwa siku hiyohiyo inapotolewa; hataacha hata sehemu yake hadi asubuhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu cho chote mpaka asubuhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwa ajili ya shukrani italiwa siku hiyo hiyo ya matoleo yake; asisaze yoyote hata asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumshukuru Mungu italiwa siku hiyohiyo inapotolewa; hataacha hata sehemu yake hadi asubuhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo nyama za hiyo ng'ombe ya tambiko ya shukrani iliyo ya sifa na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, wasiziweke mpaka kesho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwa ajili ya shukrani italiwa siku iyo hiyo ya matoleo yake; asisaze yo yote hata asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumushukuru Mungu itakuliwa siku hiyohiyo inapotolewa. Hataacha hata sehemu yake mpaka asubui.