Leviticus 7:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya nadhiri au ya hiari, italiwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu nyingine yaweza kuliwa kesho yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini ikiwa sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya nadhiri au ya hiari, italiwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu nyingine yaweza kuliwa kesho yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini cho chote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya nadhiri au ya hiari, italiwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu nyingine yaweza kuliwa kesho yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiitoa hiyo ng'ombe yake ya tambiko kwa ajili ya kiapo au kwa mapenzi yake mwenyewe, nyama zake hiyo ng'ombe ya tambiko na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, hata kesho yake masao yake yatalika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya kutimiza kiapo au ya mapenzi mema, itakuliwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu ingine inaweza kukuliwa kesho yake.