Leviticus 7:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena nyama yoyote ya sadaka ya amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitapokelewa kwa faida yake mtu aliyeitoa. Nyama hiyo ni chukizo na mtu atakayeila atawajibika kwa uovu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, Mwenyezi Mungu hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kama nyama yo yote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena nyama yoyote ya sadaka ya amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitapokelewa kwa faida yake mtu aliyeitoa. Nyama hiyo ni chukizo na mtu atakayeila atawajibika kwa uovu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama nyama yo yote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, BWANA hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi, mtu atakayekula sehemu yake yo yote atakuwa na hatia kwa uovu huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, bwana hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kama nyama yoyote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena nyama yoyote ya sadaka ya amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitapokelewa kwa faida yake mtu aliyeitoa. Nyama hiyo ni chukizo na mtu atakayeila atawajibika kwa uovu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama nyama za ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani zingeliwa siku ya tatu, mwenye kuitoa asingependeza, wala asingewaziwa kuwa mwenye kuitoa, ila zitakuwa machukizo tu, naye kila mtu atakayezila atakuwa amekora manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kama nyama yo yote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani inakuliwa kwa siku ya tatu, mutu aliyeitoa hatakubaliwa, wala hiyo sadaka haitapokelewa kwa faida yake. Nyama hiyo ni chukizo na mutu atakayeikula atabeba lazima ya uovu wake.