Leviticus 7:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnyama wa sadaka ya kuondoa hatia atachinjiwa mahali wanapochinjiwa wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na damu yake itarashiwa madhabahu pande zake zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnyama wa sadaka ya kuondoa hatia atachinjiwa mahali wanapochinjiwa wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na damu yake itarashiwa madhabahu pande zake zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnyama wa sadaka ya kuondoa hatia atachinjiwa mahali wanapochinjiwa wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na damu yake itarashiwa madhabahu pande zake zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali hapo, wanapozichinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, papo hapo na wazichinje nazo ng'ombe za tambiko za upozi, nazo damu zao na azinunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyama wa sadaka kwa ajili ya kosa atachinjiwa pahali wanapochinjiwa nyama wa sadaka za kuteketezwa kwa moto na damu yake itanyunyizwa juu ya mazabahu pande zake zote.