Leviticus 7:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na wanyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yo yote, lakini kamwe msiyale.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mafuta ya nyama aliyekufa kibudu nayo mafuta ya nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine mtayatumia ya kazi yo yote, lakini kula msiyale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mafuta ya nyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya nyama aliyeuawa na nyama wa pori yanaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini musiyakule.