Leviticus 7:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa mikono yake mwenyewe ataileta sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za BWANA kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atavileta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mikono yake mwenyewe na iyapeleke yatakayochomwa kwa moto wa Bwana, ni mafuta pamoja na kidari; akiyapeleka haya, kidari na wakipitishe motoni mbele ya Bwana, kiwe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atamuletea kwa mikono yake mwenyewe kama vile sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kilali ambacho atafanya nacho kitambulisho cha kumutolea Yawe.