Leviticus 8:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamchinja huyo ng'ombe, akachukua damu akazipaka pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake kuitakasa. Kisha akachukua damu iliyobaki akaimwaga chini kwenye tako la madhabahu ambayo aliweka wakfu kwa kuifanyia ibada ya upatanisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kutakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. Kwa hiyo akayaweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamchinja huyo ng'ombe, akachukua damu akazipaka pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake kuitakasa. Kisha akachukua damu iliyobaki akaimwaga chini kwenye tako la madhabahu ambayo aliweka wakfu kwa kuifanyia ibada ya upatanisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kuitakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu, kwa hiyo akaiweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kutakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. Kwa hiyo akayaweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamchinja huyo ng'ombe, akachukua damu akazipaka pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake kuitakasa. Kisha akachukua damu iliyobaki akaimwaga chini kwenye tako la madhabahu ambayo aliweka wakfu kwa kuifanyia ibada ya upatanisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakamchinja, naye Mose akatwaa damu, akaitia kwa kidole chake katika pembe za meza ya kutambikia pande zote, akaieua hiyo meza ya kutambikia, nayo damu nyingine akaimwagia misingi ya meza ya kutambikia, akaieua nayo, ajipatie upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamuchinja huyo ngombe, akatwaa damu akapakaa pembe za mazabahu pande zote kwa kidole chake kwa kuitakasa. Kisha akatwaa damu iliyobaki akaimwanga chini kwenye tako la mazabahu ambayo alitakasa kwa kuifanyia ibada ya upatanisho.