Leviticus 8:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, akachukua mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbo yake, sehemu bora ya ini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya madhabahu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Musa akachukua mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani, na kipande kirefu cha ini, na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, akayateketeza juu ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akayatwaa mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo yake, na kitambi kilichokuwa katika ini, na figo zake mbili, na mafuta yake, na Musa akayateketeza juu ya madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, akachukua mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbo yake, sehemu bora ya ini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya madhabahu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Mose akachukua mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake na kuyateketeza juu ya madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Musa akachukua mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, akayateketeza juu ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akayatwaa mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo yake, na kitambi kilichokuwa katika ini, na figo zake mbili, na mafuta yake, na Musa akayateketeza juu ya madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, akachukua mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbo yake, sehemu bora ya ini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya madhabahu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akayachukua mafuta yote yaliyoshikamana na utumbo na kile kipande cha ini na mafigo yote mawili pamoja na mafuta yao, kisha Mose akayachoma moto mezani pa kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akayatwaa mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo yake, na kitambi kilichokuwa katika ini, na figo zake mbili, na mafuta yake, na Musa akayateketeza juu ya madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, akatwaa mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbotumbo yake, sehemu bora ya maini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya mazabahu.