Leviticus 8:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Mose akamleta kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa. Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akamsongeza yule kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Mose akamleta kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa. Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akamsongeza yule kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Mose akamleta kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa. Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamtoa dume la kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, naye Haroni na wanawe wakaibandika mikono yao kichwani pake huyu dume la kondoo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akamsongeza yule kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Musa akaleta kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa. Haruni na wana wake wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo.