Leviticus 8:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwite Aroni na wanawe wakutane mbele ya mlango wa hema la mkutano; chukua mavazi matakatifu, mafuta ya kupaka, ng'ombe wa sadaka ya kuondolea dhambi, kondoo madume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waletee Haruni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtwae Haruni, na wanawe pamoja naye, na yale mavazi, na mafuta ya kutia, na ng'ombe mume wa sadaka ya dhambi, na kondoo waume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwite Aroni na wanawe wakutane mbele ya mlango wa hema la mkutano; chukua mavazi matakatifu, mafuta ya kupaka, ng'ombe wa sadaka ya kuondolea dhambi, kondoo madume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mletee Aroni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo waume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waletee Haruni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtwae Haruni, na wanawe pamoja naye, na yale mavazi, na mafuta ya kutia, na ng'ombe dume wa sadaka ya dhambi, na kondoo wawili wa kiume, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwite Aroni na wanawe wakutane mbele ya mlango wa hema la mkutano; chukua mavazi matakatifu, mafuta ya kupaka, ng'ombe wa sadaka ya kuondolea dhambi, kondoo madume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mchukue Haroni pamoja na wanawe na yale mavazi na mafuta ya kupaka na dume la ng'ombe atakayekuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo na madume mawili ya kondoo na kikapu cha mikate isiyochachwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtwae Haruni, na wanawe pamoja naye, na yale mavazi, na mafuta ya kutia, na ng’ombe mume wa sadaka ya dhambi, na kondoo waume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utwae Haruni na wana wake na zile nguo takatifu, mafuta ya kupakaa, ngombe wa sadaka kwa ajili ya zambi, kondoo dume wawili, na kitunga cha mikate isiyotiwa chachu.