Leviticus 8:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamchinja. Akachukua damu ya kondoo huyo na kumpaka Aroni kwenye ncha ya sikio lake la kulia, kidole gumba cha mkono wake wa kulia na cha mguu wake wa kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akamchinja yule kondoo dume, akaichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Haruni, na juu ya kidole gumba cha mkono wake wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akamchinja; na Musa akatwaa katika damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la Haruni, na katika chanda chake cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kuume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamchinja. Akachukua damu ya kondoo huyo na kumpaka Aroni kwenye ncha ya sikio lake la kulia, kidole gumba cha mkono wake wa kulia na cha mguu wake wa kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akamchinja yule kondoo dume na kuichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Aroni na juu ya kidole gumba cha mkono wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wa kuume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akamchinja yule kondoo dume, akaichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Haruni, na juu ya kidole gumba cha mkono wake wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akamchinja; na Musa akatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la Haruni, na katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole gumba cha mguu wake wa kulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamchinja. Akachukua damu ya kondoo huyo na kumpaka Aroni kwenye ncha ya sikio lake la kulia, kidole gumba cha mkono wake wa kulia na cha mguu wake wa kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akamchinja, akatwaa damu kidogo, akampaka Haroni pembe ya chini ya sikio lake la kuume na kidole gumba cha mkono wake wa kuume nacho cha mguu wake wa kuume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akamchinja; na Musa akatwaa katika damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la Haruni, na katika chanda chake cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kuume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamuchinja. Akatwaa damu ya kondoo huyo na kumupakaa Haruni kwenye incha ya sikio lake la kuume, kidole gumba cha mukono wake wa kuume na cha muguu wake wa kuume.